NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema hawatarudia makosa ambayo walifanya 2021 walipokutana na Rivers United kwenye mashindani ya kimataifa.
Septemba 12 2021 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United na ule wa pili ubao ulisoma Rivers United 1-0 Yanga ilikuwa ni Septemba 19.
Kocha huyo ameiongoza Yanga kwenye mchezo wa wa kwanza wa robo fainali ugenini na ubao umesoma Rivers United 0-2 Yanga na mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele mwenye mabao matano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia hatua ya makundi.
Nabi amesema:”Dhamira kubwa ni kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza na kutorudia makosa ambayo tulifanya wakati uliopita tulipokutana nao nakumbuka 2021.
“Ule ulikuwa wakati mwingine na sasa ni wakati mwingine tunaingia uwanjani kutafuta matokeo mazuri kwa kufuta makosa ambayo yalipita kwenye mechi zetu,” .
Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Rivers United Aprili 30,2023 mchezo wa robo fainali ya pili unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa