MASTAA wawili ndani ya kikosi cha Azam FC kwenye safu ya ushambuliaji wanaandaliwa kuimaliza Simba kwenye hatua ya nusu fainali.
Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga ambao walipata ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa fainali.
Ni nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 6,2023 pale Uwanja wa Nangwanda,Mtwara.
Ikumbukwe kwamba Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala ilitinga hatua ya nusu fainali kwa kuwatungua mabao 2-0 Mtibwa Sugar na Simba ilitinga hatua ya nusu fainali kwa kuitungua mabao 5-1 Ihefu mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo uliopita wa Azam FC kwenye ligi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri ukisoma Ruvu Shooting 1-3 Azam FC huku wafungaji wakiwa ni Ayoub Lyanga aliyefunga mabao mawili na Sopu alitupia bao moja.
Washambuliaji Mbombo na Dube walitoa pasi mojamoja za mabao kwenye mchezo huo jamb lililompa furaha Ongala.
Ongala amesema:”Dube na Mbombo hawa wote ni wachezaji wazuri na mechi ijayo ni dhidi ya Simba tunaamini kwamba yule atakayepewa nafasi ataonyesha uwezo wake,”.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imetinga hatua ya nusu fainali pia itamenyana na Singida Big Stars kwenye mchezo wao ujao.