AZAM FC YAIPIGA MKWARA SIMBA

KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni mchezo wao wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba.

Taji hilo la Kombe la Azam Sports Federation mabingwa watetezi ni Yanga ambao nao wametinga hatua ya nusu fainali.

Itacheza na Singida Big Stars Uwanja wa Liti na mshindi wa mchezo wao atakutana fainali na mshindi wa mchezo wa Azam FC v Simba.

Ni nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 6,2023 Uwanja wa Nangwanda,Mtwara.

Azam FC ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na Simba ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 5-1 Ihefu mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ongala amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na timu zote kuwa bora na zinahitaji ushindi.

“Mchezo wetu dhidi ya Simba hautakuwa mwepesi kwani kila timu inahitaji ushindi kutokana nasi tunafanya maandalizi katika mchezo wetu ambao unatukabili.

“Ushindi wetu dhidi ya Ruvu Shooting umetupa nguvu kwa ajili ya mechi hiyo kwani vijana walicheza vizuri na kupata matokeo hivyo ni kazi kwetu kuendelea pale ambapo tuliishia,”