KAZI BADO IPO KWENYE LIGI, HAKUNA KUKATA TAMAA

KUKATA tamaa kwenye mechi za mzunguko wa pili kwa wachezaji wa timu ambazo zimekwama kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao iwe ni mwiko.

Bado kuna kazi ya kufanya na kwenye mpira lolote linaweza kutokea kutokana na namna ambavyo timu zitajipanga kwa umakini licha ya kwamba Yanga inaongoza haina maana kwamba ligi imeshagota mwisho.

Tunaona mzunguko wa pili huu ni muda wa kukamilisha hesabu na kila timu inatimiza jambo lake kwa namna tofauti.

Zipo ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja na hazijawa kwenye mwendo mzuri kutokana na kushindwa kupata matokeo chanya hilo lipo wazi.

Wachezaji wanaonekana wameanza kukata tamaa licha ya kwamba wana mechi mkononi za kucheza ambazo wanaziona labda ni chache pengine.

Ukweli ni kwamba kwenye ulimwengu wa mchezo kila mchezaji anapaswa kuelewa kwamba haitakuwa mwisho mpaka itakapokuwa mwisho.

Jambo la muhimu ni kufuata maelekezo kutoka kwenye benchi la ufundi na kuyafuata kwa umakini kwani inawezekana na muda ni sasa.

Kuhusu kuwama kushindwa kupata matokeo benchi la ufundi linajua wapi wanapaswa kuboresha ili wakati ujao wawe imara hasa katika ngwe ya mwisho.

Tunaona vita ya tatu bora ni ngumu kwa Singida Big Stars v Azam FC hawa wote wana mechi mkononi hivyo acha kazi iendelee.

Pale ambapo wanaona kazi inakuwa ngumu wanapaswa kubadili mbinu kwa wachezaji ambazo zitawapa nguvu ya kusaka matokeo uwanjani.

Pointi tatu kwa mechi za mwisho sio rahisi kuzipata lakini inawezekana kuzipata kukiwa na mpango kazi kwa ajili ya kushinda mechi hizo ambazo ni ngumu.