YANGA YASHUSHA 5 G

HUU ni ushindi mkubwa kwa Yanga kwa msimu wa 2022/23 dhidi ya Kagera Sugar wakisepa na pointi tatu mazima.

Ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Yanga 5-0 Kagera Sugar baada ya dakika 90 kukamilika.

Aziz KI kasepa na mpira wake kwa kuwa amefunga mabao matatu, mawili kwa penalti dakika ya 43 na 90 huku lile la dakika ya 45 akipachika kwa shuti akiwa nje ya 18.

Fiston Mayele kajaza kimiani bao moja dakika ya 49 na Bernard Morrison katupia dakika ya 84.

Kituo kinachofuata ni dhidi ya Simba, Aprili 16 2023, Uwanja wa Mkapa.