MIAMBA HII IMEKIMBIZA KINOMA KIMATAIFA

MIAMBA wawili wazawa, Mudhathir Yahya na Farid Mussa wamefunga hatua za makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa na rekodi ya kila mmoja kuwatungua TP Mazembe.

Hawa ni wazawa wawili ambao wametupia mabao kwenye hatua ya makundi wakati Yanga ikitinga hatua ya robo fainali.

Nyota wote wameitungua TP Mazembe ambapo wa wanza kufunga alikuwa ni Mudhathir Yahya kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Yanga 3-1 TP Mazembe.

Mchezo wa pili ugenin, Mudhathir alianza na alimpisha Farid dakika ya 54 akatumia dakika 8 kufunga bao lake la kwanza katika hatua ya makundi ilikuwa dakika ya 63.

Yanga ikiwa imefunga mabao 9 hatua ya makundi mabao 7 yamefungwa na wachezaji wakigeni, Fiston Mayele raia wa DR Congo yeye katupia matatu, Kennedy Musonda raia wa Zambia katupia mabao mawili huku Tuisila Kisinda na Jesus Moloko hawa wote raia wa DR Congo wakiwa wametupia mojamoja.