Uwanja wa Highland Estate Mbeya unapigwa mchezo wa kiume katika msako wa pointi tatu muhimu.
Ubao unasoma Ihefu 0-0 Simba huku kila timu ikifanya mashambulizi kwa zamu.
Ihefu wanaonekana kuwa bora katika umiliki wa mpira na kufanya majaribio langoni mwa Simba ambapo amekaa Ally Salim.
Simba wanamtumia Kibu Denis, Jean Baleke kufanya mashambulizi huku Ihefu wakiwa na Yacouba Songne, Obrey Chirwa.
Fikirini Bakari yupo kwenye lango la Ihefu naye akipambania kuweka ngome salama