VIGOGO WAMEPATA TABU MBEYA

WAKATI leo Ihefu wakitarajiwa kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili rekodi zinaonyesha kuwa vigogo wengi wa Dar wamebuma kusepa na pointi tatu.

Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, John Simkoko na Zuberi Katwila ambaye ni msaidizi imekuwa na mwendo bora kwa mechi wanazocheza nyumbani.

Yanga wao kete yao ya kutofungwa mechi 50 ilibuma hapo baada ya ubao kusoma Ihefu 2-1 Yanga ilikuwa ni Novemba 29,2023.

Hivyo Yanga walikwama kuendeleza rekodi ya kutofungwa kwenye mechi za ligi baada ya kucheza mechi 49 mfululizo bila kufungwa.

Matumaini ya Azam FC kutwaa taji la ligi yalizimikia kwenye uwanja huo baada ya ubao kusoma Ihefu 1-0 Azam ilikuwa ni Machi 13,2023.

Simba leo wana kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye Uwanja wa Highland Estate ambao una rekodi ya kutibua mwendo kwa vigogo hivyo dakika 90 zitaamua kama rekodi itavunjwa na Simba ama rekodi itaendelea kwa timu kutoka Simba