SIMBA NDANI YA MBEYA KUIKABILI IHEFU

KIKOSI cha Simba kimewasili Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Highland Estate Mbeya Jumatatu, Aprili 9,2023.

Simba imetoka kupata ushindi wa mabao 5-1 Ihefu kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali.

Mchezo huo wa ligi utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa Ihefu wawapo nyumbani.

Ikumbukwe kwamba Azam FC, Yanga hazikutoka salama kwenye uwanja huo kwenye mechi za ligi.

Imeongozana na Juma Mgunda, Roerto Oliveira ambao wapo kwenye benchi la ufundi.

Jean Baleke, Pape Sakho, Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo.