YANGA 0-0 GEITA GOLD

UBAO wa Uwanja wa Azam Complex mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Azam Sports Federation ngoma ni nzito.

Hakuna mbabe ambaye amepata bao la kuongoza ubao unasoma Yanga 0-0 Geita Gold.

Moja ya mchezo ambao una ushindani mkubwa ambapo ni nyota Clement Mzize pekee ameonyeshwa kadi ya njano.

Kadi hiyo imezua maswali kutokana na kile ambacho kilionekana Mzize kuchezewa faulo na mchezaji wa Geita Gold.

Ni mashuti manne Yanga wamepiga yamelenga lango huku Geita Gold wakipiga shuti mojalililolenga lango.

Kwa upade wa mapigo huru Kisinda Tuisila mzee wa spidi amepewa jukumu hilo ambapo faulo yake dakika ya 41 ilikwenda nje ya lango.