NYOTA Bernard Morrison tayari yupo ndani ya uwanja wa mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Geita Gold baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akipambania hali yake.
Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza hatua ya makundi na kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho kutokana na kutokuwa fiti.
Yanga inayonolewa a Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Geita Gold.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Aprili 8 saa 2:00 usiku.
Ni robo fainali ya Azam Sports Federation na mshindi wa mchezo huo atakutana na Singida Big Stars kwenye hatua ya nusu fainali.