VITA ni kubwa kwelikweli kwenye Championship kutokana na kila timu kupambana kupata matokeo mazuri ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
Hili ni muhimu kufanyika kwakila timu kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na kwa wale ambao wamekata tamaa bado muda upo wakuzinuduka kwa sasa.
Kutokana na kila timu kuwa na mpango wa kupanda ligi kunaongeza ushindani na kufanya kila mechi kuwa fainali hii ni kubwa na bora.
Kwa kadri siku zinavyozidi kwenda ule ukubwa wa ligi hii unazidi kuwa mkubwa na unatengeneza wachezaji bora ambao wanakuwa na manufaa kwenye timu zao na jamii kiujumla.
Wakati huu kinachotakiwa kwa kila mmoja ni kufanya kazi kubwa kwenye kutafuta ushindi nah ii itaongeza thamani kwenye ligi hii.
Kwa wadau wa mpira ni muhimu kuwakumbuka hawa wanaocheza huku Championship kwani kazi yao ni kubwa na inaongeza uwanda mpana wa kuibuka vipaji.
Wapo wachezaji waliopata nafasi kucheza kwenye timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwa ni kutoka Championship na wanafanya vizuri.
Kwa maana hiyo huku vipaji vipo kinachotakiwa ni kuongeza nguvu zaidi ili kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo wa kushindana kwenye kila namna.
Wale ambao hawajawa kwenye mwendo mzuri ni wakati wao kuanza kazi kwa sasa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo zimebaki.
Muda mchache wanasema na mambo ni mengi basi nguvu kubwa iwe kwenye kusaka ushindi kila wakati kwa wachezaji wanaoshiriki Championship.