HEMED Morocco, kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kuongezeka kwa wachezaji katika kikosi hicho kunaongeza upana wa kuchagua kikosi kitakachoanza dhidi ya Uganda.
Ni Mohamed Hussein na Shomari Kapombe hawa wameongezwa katika timu ya Tanzania inayofanya maandalizi ya mwisho kuikabili Uganda.
Ni kesho Uwanja wa Mkapa saa 2:00 usiku mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo jukwaa la mzunguko ni suala la mashabiki kuwahi mapema uwanjani na kuingia kuishangilia Stars.
Morocco amesema:”Tulipata ushindi mchezo wa kwanza hilo ni jambo kubwa kwetu na sasa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu wa nyumbani.
“Uwepo wa wachezaji wengine ambao wamongezeka ikiwa ni pamoja na Kapombe na Mohamed unaongeza upana wa chaguo kwenye kikosi cha kwanza ila hata wale ambao walicheza Uganda walifanya kazi nzuri,”.
Ni Serikali imetoa tiketi 7,000 huku wadau wengine ikiwa ni pamoja na Injinia Hersi Said, Mo Dewji, Singida Big Stars ni miongoni mwa walionunua tiketi kwa ajili ya mashabiki kuishangilia Stars.