STARS WAPENI FURAHA MASHABIKI KWA KUFANYA KWELI

WAKATI mzuri kuendeleza mazuri ambayo mlifanya kwenye mchezo uliopita ugenini mkiwa na mashabiki wenu ni sasa kwa wachezaji wa Stars .

Hakika kushinda ugenini ni ushindi mkubwa mbele ya mashabiki wao waliokuwa nao hapo unadhani wao watakuwa wanahitaji nini kama sio ushindi?

Wamepata ugumu walipokuwa nyumbani sasa wanakuja ugenini wakihitaji kurejea na furaha hivyo ni muhimu kwa wachezaji kujituma.

Ili kuifanya furaha idumu ni lazima wachezaji wazidi kupambana na kuendelea kufanya kazi kusaka ushindi kwani inawezekana.

Itakuwa ni furaha zaidi kutokana na ugumu wa wapinzani ambao nao wanahitaji kupata furaha basi wachezaji ni muhimu kuongeza juhudi zaidi.

Tunaona wapo ambao wameongezwa kwenye kikosi cha Stars kuongeza nguvu basi wakipewa nafasi waendelee kufanya kazi kubwa kuendeleza ile ari ya ushindi.

Inawezekana kushinda nyumbani ikiwa mipango itakuwa mizuri na wachezaji watajituma kufuata mbinu za walimu pamoja na kupunguza makosa.

Makosa makubwa yataigharimu timu ikiwa yatafanyika na kutumia makosa ya wapinzani itakuwa ni faida kwa Stars.

Basi wakati wa kupunguza makosa kwa wachezaji ni sasa na wakati wa kutumia makosa ya wapinzani muda ni huu na Watanzania watakuwa pamoja kwenye furaha.

Ile kasumba ya kushindwa kufanya vizuri pale mnapokuwa na mashabiki isipewe nafasi bali kila mmoja apambane kupata ushindi.

Kila la kheri wachezaji muda wa mafanikio ni sasa na kila kitu kitakuwa sawa ikiwa mtajituma zaid.