KAGERA SUGAR KWENYE KIBARUA UHURU

NI kocha bora wa Februari Mecky Maxime leo Machi 9,2023 ana kibarua cha kuongoza kikosi chake dhidi ya KMC.

Kocha huyo ambaye anapenda kuona vijana wakicheza kwa kujiamini mchezo wake uliopita wa ligi alishuhudia ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 1-0 Namungo.

Ilikuwa ni Februari 18 ambapo bao pekee la ushindi lilijazwa kimiani na mzawa Eric Mwijage aliyeamilisha majukumu yake kuipa pointi tatu Kagera Sugar.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 Jioni.

Kagera Sugar kwenye msimamo wapo nafasi ya 6 ikiwa na pointi zake 32 huku KMC ipo nafasi ya 13 na pointi 23.