TANZANIA:NYOTA MTIBWA SUGAR ATANGULIA MBELE ZA HAKI

TAARIFA za awali zinaeleza kuwa nyota wa wa Mtibwa Sugar yenye maskani yake Morogoro, Iddy Mobby ametangulia mbele za haki.

Mobby amekamilisha mwendo akiwa kwenye matibabu kwenye Hospital ya Mkapa iliyopo mkoani Dodoma alipohamishiwa baada ya matibabu ya awali kwenye Hospital ya kiwanda.

Inaarifiwa kwa mujibu wa watu wa karibu na Mtibwa ni kuwa beki huyo alikuwa na maumivu ya kichwa kabla ya kupelekwa hospital.

Pumzika kwa amani