MTIBWA SUGAR WANYOOSHWA UWANJA WA LITI

IKIWA Uwanja wa Liti, Singida kwa wakulima Alizeti Mtibwa Sugar iliacha pointi zote tatu mazima.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 27,2023 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Big Stars 2-0 Mtibwa Sugar

Ni Rodrigo alianza kuwatungua Mtibwa Sugar wenye Duchu ilikuwa dakika ya 12 kisha mwamba kabisa Meddie Kagere huyu alizamisha boti dakika ya 37.

Mbinu za Mtibwa Sugar kusaka ushindi ugenini ziligota mwisho mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulisoma Singida Big Stars 2-0 Mtibwa Sugar.

Huu ni mzunguko wa pili wa lala salama ambapo kila timu inapambana kusepa na pointi tatu kwenye mechi za nyumbani na ugenini.