NGOMA NZITO KWA SIMBA, WAGAWANA POINTI NA AZAM

NGOMA nzito kwa Simba mbele ya Azam FC baada ya Mzizima Dabi kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mchezo ulioshuhudia bao la mapema na bao la usiku kwa timu zote mbili huku wafungaji wote wakitoka ndani ya Azam FC.

Ni Prince Dube alianza kuwatungua Simba dakika ya kwanza alipompa tabu Aishi Manula mpaka dakika 44 ngoma ilikuwa inasoma Simba 0-1 Azam FC.

Dakika 44 za kipindi cha pili kazi ilikuwa ngumu kwa timu zote ambapo nyota wa Azam FC Adalah Keri kwenye harakati za kuokoa hatari alijifunga bao dakika 90.

Kazi ngumu kwa Simba kazi ngumu kwa Azam FC bonge moja ya mchezo uliokuwa na matumizi makubwa ya nguvu na akili.