WANASEMA mwili haujengwi kwa mawe bali ugali na mbonga majani zile za kutoka shambani, ikitokea umekwama kuingia shambani basi tarajia kukosa kuujenga mwili.
Weka kando hayo kuna shamba la ushindi ambalo wengi wanatarajia kuliona leo ndani ya dakika 90, Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya TP Mazembe.
Ikumbukwe kwamba Februari 12 ubao wa Uwanja wa Olympique de Rades ulisoma US Monastir 2-0 Yanga ni Mohamed Saghroui dakika ya 10 ilitokana na pigo la faulo na lile la pili lilifungwa na Boubacar Traore dakika ya 15.
Yanga wakiwa hawajakusanya pointi kwa kuwa waliziacha Tunisia kwa wapinzani wao US Monastir hapa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amebainisha hesabu za timu hiyo namna hii:-
“Ipo wazi kwamba mchezo wa kwanza tulipoteza ugenini na tumerudi nyumbani kwa ajili ya kuendelea kusaka ushindi kwa kuwa mechi bado hazijaisha.
“Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kusahau matokeo ambayo yamepita n ahata tukikumbuka hakuna ambaye anaweza kuyabadili hivyo kazi yetu ipo kwenye maandalizi ya mchezo wetu wa nyumbani.
Kwa wachezaji hali ipoje?
“Ni majukumu yao kuwa tayari kuendelea kuipambania nembo ya Yanga na wapo tayari kufanya hivyo muda wote ndio maana wamesajiliwa kwenye kikosi.
“Kila mmoja anapenda kuonyesha kile ambacho wengi wanahitaji kuona amacho ni matokeo mazuri. Matokeo mazuri yanatona na ushirikiano ambao upo kwa kila mchezaji hilo lipo sawa.
Wapinzani wenu mnawatazamaje?
“Ni timu ambayo inashiriki mashindano ya kimataifa haijafika hapo kwa bahati mbaya inamaanisha kwamba nit mu nzuri nasi tunalitambua na tunawaheshimu.
“Tutaingia kwa tahadhari kubwa kwenye kutafuta ushindi jambo hili linawezekana kwa kuwa mpira una njia zake na mbinu zake hilo litafanyiwa kazi na benchi la ufund.
“Kupitia namna ambavyo wamewasoma wapinzani kwenye mechi zao zilizopita inamaanisha kwamba mbinu zao zinafahamika na wakati wa mchezo ni muda wa kusaka ushindi mbele ya wapinzani wetu ambao wanakuja nyumbani.
Kwa nini Super Sunday?
“Hakuna mchezo mwingine mkubwa ambao utachezwa Jumapili hapa itakuwa ni Yanga kwenye mechi yetu ya kimataifa ambayo itakuwa na utofauti wa kipekee.
“Hapo tunafanya kwa ajili ya kila mmoja kupata muda wa kuwaona Wananchi wakitoa burudani pamoja na kusaka ushindi kwenye mchezo wetu ambao ni muhimu kupata ushindi.
Kupoteza mchezo wa kwanza kumewatoa kwenye reli?
“Haiwezi kuwa hivyo kwa kuwa ni mchezo mmoja ambao tumecheza na kuna mechi nyingine zinakuja nazo zinatuhusu ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya TP Mazembe.
“Malengo bado hayajafika mwisho kwa kuwa kazi inaendelea na tunaamini tutafanya vizuri kwenye mechi zijazo kutokana na benchi la ufundi kuwa makini na wachezaji kuwa na morali kubwa kwenye kusaka ushindi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza.
“Matokeo kwenye mpira haina maana kushindwa kuendelea na mipango mikubwa ni kupata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kazi inaendelea.