MCHEZO wake wa kwanza ikiwa Uwanja wa Mkapa kwenye anga za kimataifa kwa mwaka 2023 inapoteza.
Ni kipigo kinachovunja rekodi yake tamu ya kutofungwa ikiwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 kusoma Simba 0-3 Raja Casablanca.
Kipindi cha kwanza Raja Casablanca walianza kwa utulivu mkubwa na walipata bao moja la kuongoza huku Simba wakikosa umakini kwenye kumaliza nafasi mbili za dhahabu walizotengeneza.
Ngoma ilikuwa nzito kipindi cha pili ambapo Raja iliwatungua Simba mabao mawili moja likiwa kwa mkwaju wa penalti uliomshinda Aishi Manula.
Mwanzo mbovu kwa Simba ikiwa haijakusanya pointi kwenye hatua ya makundi.
Raja wameonyesha kuwa uwekezaji wao sio uwanjani kwani licha ya kuwa ni wachache kwa upande wa mashabiki wliokuja walishangilia kwa mpango kazi mkubwa jambo ambalo ni somo kwa mashabiki wetu.
Huu ni mchezo wa pili kwa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kupoteza baada ya ule wa awali kunyooshwa bao 1-0 dhidi ya Horoya.