BEKI wa kati wa Yanga, Yannick Bangala amesema wanafahamu mchezo wao dhidi ya TP Mazembe utakuwa na upinzani mkubwa lakini watahakikisha kuwa wanapambana ili waweze kupata matokeo ya ushindi wakiwa nyumbani.
Bangala amewahi kukipiga AS Vita anawafahamu vyema TP Mazembe jambo ambalo ni faida kubwa kwa Yanga kuelekea katika mchezo huo.
Yanga Jumapili February 20 watawaalika TP Mazembe Uwanja wa Mkapa kwaajili ya mchezo wa pili wa kundi D ikiwa ni michuano ya kKombe la Shirikisho Afrika.
Bangala amesema kuwa wao binafsi kama wachezaji wanatambua ubora wa TP Mazembe jambo ambalo nilazima wapambane ili kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi ambayo yatakuwa na faida kubwa kuelekea kupata mafanikio.
“TP Mazembe tunawafahamu vyema tangia tukiwa DR Congo,ni timu nzuri na ukiangalia tunafahamiana vyema sisi wachezji wa Yanga ambao tumetoka kule Congo na wao wanatufahamu sisi vyema hivyo itakuwa ni mechi nzuri na yenye ushindani mkubwa kwa upande wote.
“Kwetu sisi ambacho tunajiandaa nacho ni kuhakikisha kuwa tunashinda kwa kuwa ndio mchezo wetu wa kwanza tukiwa nyumbani na isitoshe tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunashinda ili tutengeneze mazigira bora ya kuvuka kwenda hatua inayofuata ya robo fainali,tutapambana kupata matokeo,” amesema.