MASHINDANO ya vijana wa shule za Afrika Mashariki (CECAFA) yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi leo Ijumaa katika Uwanja wa Azama Complex Chamanzi.
Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu yanashirikisha jumla ya nchi nane kutoka Afrika mashariki na kati huku Tanzania akiwa ndio mwenyeji wa michuano hiyo.
Hizi ni mechi za Kanda za kufuzu kwa Michuano ya CAF AfricanSchool Football na itakuwa mubashara kupitia Global TV Online pekee kwa Tanzania.
Ni wenye umri wa kati ya miaka 12-15 watakaocheza kwa upande wa wavulana na wasichana huku kwa wavulana kukiwa na timu nane kwa upande wa wasichana zikiwa timu saba.
Timu shiriki ni pamoja na Tanzania, Djibout, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Uganda, Burundi,Ethiopia.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu ambapo ni Ijumaa February 18,Jumamosi na kutamatika Jumapili ya February 20.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Wilfred Kidao amesema kuwa ni furaha kubwa kuaandaa mashindano hayo ya CAF.
“Tunafuraha kubwa kuandaa mashindano mengine ya CAF nchini. Tumewahi kuandaa mashindano mengine ya CAF a kila tunapoandaa hutusaidia kuendelea kujifunza mambo mapya,”.