TRY AGAIN USO KWA USO NA RAIS FIFA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino akiwa na Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene baada ya kushiriki moja ya vipindi vinavyoendelea kwenye kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management).

Kozi hiyo inafanyika mjini Tangier, Morocco.

Try Again ni mmoja wa wajumbe watatu kutoka Afrika ambao wanashiriki kozi hiyo ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki amechaguliwa yeye.

Huu ni mwendelezo wa FIFA kutoa kozi hiyo kwani ilianzia nchini Qatar wakati Kombe la Dunia likiendelea ambako pia Try Again alishiriki.