AZAM FC KUKIWASHA LEO MECHI YA KIMATAIFA

LEO Uwanja wa Azam Complex, Azam FC itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ikiwa ni kwa ajili ya kujipima timu hiyo ambayo imetinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho.

Azam FC ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-1 Dodoma Jiji.

Ofisa Habari wa Azam FC,Hasheem Ibwe amesema kuwa maandalizi ya mchezo wao yapo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani.

“Wachezaji wapo tayari na maandalizi ambayo tumefanya yapo sawa tunaamini kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mchezo wetu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya mchezo wetu muhimu na tuna amini tutawapa burudani na furaha pia,”.

Januari 30 2023 Azam FC ilifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi hayo ni Rodgers Kola, Sopu, Prince Dube.