JANUARI 30,2023 Yanga imezindua uzi wao mpya kwa ajili ya mechi za kimataifa ikiwa imetinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Februari 12 ina kibarua kwenye mchezo wa kimataifa.
Kabla ya kusepa Bongo bado itakuwa na kazi ya kucheza mchezo mmoja wa ligi itakuwa dhidi ya Namungo FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Februari 4, kisha watasepa kuelekea Tunisia.
Ni Februari 12,2023 Yanga inatarajiwa kumenyana na Monastri ikiwa ni mchezo wao wa kwanza mwaka huu kwenye hatua ya makundi.