UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya kikosi cha Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Ni Januari 28,2023 ambayo ni Jumamosi utapigwa mchezo huo Uwanja wa Mkapa.
Ally amesema:”Wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Coastal Union ambapo kila mchezaji yupo tayari.
“Clatous Chama, Ismail Sawadogo, Jean Baleke wapo tayari kwa mchezo na Peter Banda pia yupo tayari ikumbukwe kwamba walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji,” amesema.