KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting, Cedrick Kaze kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo.
Kesho Yanga inatarajiwa kumenyana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.
Cedrick amesema wanatamua utakuwa ni mchezo mgumu lakini wapo tayari ili kupata matokeo chanya.
“Wachezaji wana morali nzuri kuelekea mchezo huo na tunaamini tunaenda kucheza mchezo mzuri utakaotusaidia kupata alama tatu muhimu,”
Mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda mabao 2-1 Uwanja wa Mkapa na kusepa na pointi tatu muhimu.