KIKOSI cha Simba kimewasili Dodoma,makao makuu ya Tanzania leo Januari 20,2023.
Chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliviera kikosi hicho kilianza safari mapema leo mchana kutoka Dar.
Mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa Oliviera baada ya ule wa kwanza kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 3-2 Mbeya City.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni Erasto Nyoni, Saidi Ntibanzokiza, Beno Kakolanya, Aishi Manula na Ally Salim.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Januari 22, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.