CHUMA KIPYA CHATAMBULISHWA IHEFU FC

ADAM Adam nyota wa zamani wa kikosi cha JKT Tanzania kwa sasa atakuwa ni mali ya Klabu ya Ihefu.

Nyota huyo anaibukia ndani ya Ihefu FC akitokea kikosi cha Mtibwa Sugar chenye maskani yake pale Morogoro.

Leo Januari 11,2023 Ihefu wamemtambulisha rasmi mshambuliaji huyo.

Ni moja ya washambuliaji wazawa wenye uwezo mkubwa uwanjani na alikuwa ni chaguo la kwanza ndani ya Mtibwa Sugar.

Huenda akawa sehemu ya kikosi cha Ihefu FC kitakachokabiriana na Yanga, Jumatatu Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa ligi.