UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwenye dirisha dogo la usajili wanashusha wachezaji wawili wa kazi kwa ajili ya timu hiyo kuboresha kikosi chao.
Ni Nasreddine Nabi anakinoa kikosi hicho ambacho kinaongoza ligi kikiwa na pointi 50 kibindoni na mtupiaji wao namba moja ni Fiston Mayele mwenye maao 14.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanaleta wachezaji wawili ambao watakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwenye kikosi hicho.
“Tunamleta beki ambaye huko alikotoka ilikuwa timu yake ikipata kona mashabiki wake wanashangilia, anapenda kona kuliko penalti.
“Mshambuliaji anayekuja, timu kubwa kutoka Misri,Afrika Kusini zilipomuulizia akawajibu mimi ni Mwananchi,” Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga.