NAHODHA wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk anayecheza hapo kwa mkopo akitokea Fernebache ya Uturuki Mbwana Samatta amefunguka kuwa, siyo ajabu siku moja akwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Samatta aliyasema hayo wakati alipohojiana na Salama Jabir kwenye kipindi cha Salama Na, aliweka wazi kuwa yeye ana uchu wa mafanikio na huwa anapata maumivu akiona Taifa Stars inafanya vibaya na uona kuna vitu inawezekana kufanyika.
Samatta alisema: “Mimi nina uchu sana wa mafanikio na kuna wakati ni kitu ambacho huwa kinatembea sana kwenye akili yangu, hadi mke wangu anajua na huwa ananiambia, kwanini kila wakati nawaza mambo hayo tu.
“Kusema ukweli uwa naumia sana ninapoona timu ya taifa inapofanya vibaya, huwa naona kama kuna vitu vinaonekana kama huwa vinawezekana kufanyika.
“Kwahiyo inawezekana siku moja, nikafanya hiyo na siyo ajabu nikaenda huko.”