BANDA ANAREJEA MDOGOMDOGO

NYOTA wa Simba, Peter Banda anaendelea na program maalumu itakayomrejesha kwenye ubora wake.

Mchezaji huyo hajaonekana uwanjani kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na ushindani kwa muda mrefu baada ya kupata maumivu.

Ni kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars alipata maumivu alipoingia akitokea benchi na alifunga bao moja.

Ngoma ilikuwa nzito katika mchezo huo kwa kuwa waligawana pointi mojamoja kwa kufungana bao 1-1.

Banda yupo nchini Dubai na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Robertinho Oliviera raia wa Brazil akishirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.

Ilikuwa ni Novemba 9 2022 mchezo huo ulipochezwa Uwanja wa Liti.