BAADA ya Kelvin Nashon kusepa ndani ya Geita Gold na kuibukia Singida Big Stars nyota mwingine anatajwa kusepa ndani ya kikosi hicho.
Ni mshambuliaji ambaye ni nahodha pia Danny Lyanga anatajwa kuibukia Dodoma Jiji.
Lyanga ni mshambuliaji hivyo anakwenda kuongeza nguvu Dodoma Jiji ambayo imefunga mabao 14 kwenye mechi 19.
Wengine waliosepa Geita Gold ni Said Ntibanzokiza huyu yupo Simba, Juma Mahadhi yupo Coastal Union.
Wengine ni Adeyoum Saleh yupo Dodoma Jiji na Ramadhan Chombo anayetajwa kuwa kwenye hesabu za Polisi Tanzania.
Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro ambaye ni mzawa.
Timu hiyo ipo kwenye hesabu za kuboresha kikosi hicho ili kuwa imara kwenye mashindano ambayo wanashiriki.