KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba
Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 7,2023 na TFF baada ya jana Januari 6,2023 shauri hilo kusikilizwa makao makuu ya TFF.
Kwenye taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi kwa pande zote mbili zilikuwa zinahusika kwenye shauri hilo utatolewa Jumatatu, Januari 9,2023 Jumatatu.
Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji wao Feisal Salum kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha.
Kamati hiyo ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo pande zote mbili ziliwakilishwa na wanasheria wao.