BEKI LA KAZI AZAM FC LINAPIGIWA RADA NA TIMU KIBAO

MOJA ya mabeki ambao wanatazamwa kwa ukaribu na timu za Kariakoo pamoja ana nje ya nchi ni pamoja na mwamba huyu Daniel Amoah mali ya Azam FC.

Novemba 6,2021 aliweka wazi kuwa bado stori yake na maisha ndani ya Azam FC yanaendelea.

Amoah amekuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala ambaye amekuwa na mwendo mzuri katika kikosi hicho.

Kwa sasa timu hiyo inashiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2023 na imetinga hatua ya nusu fainali ikiwa imekusanya pointi nne kibindoni.

Alianza kikosi cha kwanza wakati wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri na hakuanza kwenye mchezo waliotoshana nguvu na Malindi.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wana uwezo mkubwa kwenye kutimiza majukumu yao.

“Kila mchezaji anatimiza majukumu yake na kila mmoja anafurahia maisha ndani ya kikosi na ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuendelea kutazama wale ambao tutahitaji kufanyia maboresho kwa kuwa kazi bado inaendelea,”.