JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa aliteleza kwenye maelezo wakati akizingumza kuhusu suala la kutetea ubingwa wa timu hiyo.
Kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Mlandege, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuvuliwa ubingwa, alipohojiwa na mwandishi kuhusu matumaini ya kutetea taji hilo alibainisha bado yapo kwa kuwa wana mechi mbili.
Jamo hilo lilizua gumzo kutokana na ukweli kwamba mechi ambazo wanapaswa kucheza kwenye kundi ni mbili kwa kuwa timu zipo tatu.
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ ukiwa ni mchezo wao wa mwisho na leo wanarejea Dar, Mgunda amesema”Mimi ni binadamu kama binadamu wengine nilisema nilichanganya kama ilivyo binadamu wengine.
“Nilichanganya mechi mbili hiyo ilikuwa ni pamoja na ile ambayo tuliipoteza lakini mimi ni binadamu kama binadamu wengine nilikuwa najua kuhusu mechi ambazo tutacheza lakini niliteleza.
“Nilikuwa ninajua mechi ni mbili sasa katika maelezo niliteleza, nisaidie katika kurekebisha kwa hilo ambalo lilitokea ninaomba radhi kwa kuwa mimi ni binadamu na niliwaambia waandishi wengine kuhusu suala hili.
“Katika hilo nilikosea na mashabiki niliwachanganya kwa kweli ukweli ni huo kwa yaliyotokea kwenye mashindano haya nilikuwa ninajua kwenye kila timu ni timu moja inapita,” amesema Mgunda