CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga ameweka wazi kuwa mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars hautakuwa mwepesi hivyo wataingia kwa nidhamu.
Ni mchezo wa pili kwenye Kombe la Mapinduzi Yanga watacheza leo Januari 6,2023 baada ya ule wa kwanza kukamilisha kwa ushindi.
Katika mchezo wa ufunguzi Yanga ambayo inamtumia Yacouba Songne kwenye mashindano hayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM.
Bao la ushindi lilifungwa dakika ya 90 na nyota Dickosn Ambundo ambaye katika dakika za mwanzo alikosa nafasi za wazi zaidi ya mbili.