MWAMBA HUYU HAPA MFUNGAJI WA BAO LA KWANZA SIMBA

LIKUMBUKE hili jina la Michael Joseph nyota wa kikosi cha Simba kutoka timu B anakuwa wa kwanza kufunga bao ndani ya timu hiyo kwa mwaka 2023.

Ni kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 ambapo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imevuliwa mazima ubingwa wao.

Kwenye mchezo wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-0 Mlandege jambo lililoyeyusha matumaini ya timu hiyo kutetea ubingwa wake mwaka 2023.

Katika mchezo wa hitimisho dhidi ya KVZ walipata ushindi wa bao 1-0 ambapo mfungaji alikuwa ni Joseph.

Ilikuwa ni dakika ya 41 bao hilo la ushindi kwa Simba lilipatikana na kuipa pointi tatu muhimu.

Kwenye msimamo wa kundi C Simba nagotea nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu huku Mlandege wakiwa ni namba moja na pointi 4 kibindoni.

Mlandege wanatinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2023.

Kikosi cha Simba kitarejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho bila kusahau Ligi ya Mabingwa Afrika.