ROBERTINHO Oliviera raia wa Brazil anatajwa kumalizana na mabosi wa Simba kwa ajili ya kupewa mikoba ya Zoran Maki.
Ikumbukwe kwamba baada ya Maki kusepa ndani ya kikosi cha Simba mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 alikabidhiwa timu Juma Mgunda ambaye alitajwa kuwa atakuwa ni kocha mkuu wa muda.
Kocha huyo alikuwa anainoa timu ya Vipers ya Uganda ambapo alibwaga manyanga hivi karibuni ndani ya timu ya timu hiyo.
Leo kikosi cha Simba kinatarajiwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi 2023 ambapo Simba ni mabingwa watetezi.
Kuhusu suala la kocha mpya, Ahmed Ally, meneja wa idara ya habari, Ahmed Ally amesema kuwa mashabiki wawe watulivu wafurahie huduma ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda.
“Mashabiki wawe na subira kwa sasa tupo na Juma Mgunda, kocha wa mabao kocha ambaye amepata ushindi kwenye mechi zake nyingi kwa ushindi mkubwa hivyo acha tufurahie ushindi,”.