LICHA ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma KMC 1-3 Simba, bado safu za ulinzi kwa timu hizi mbili zina kazi ya kuongeza nguvu kwa ajili ya kupata matokeo kwa mechi zijazo.
Bao la kwanza KMC ilitunguliwa kupitia kwa John Bocco dakika ya 15 na kwa upande wa KMC wao ni mali ya Sadala Lipangile ambaye alipachika bao hilo dakika ya 51.
Bao la pili lilipachikwa na Okra dakika ya 54 akitumia mpira uliotemwa na David Mapigano katika harakati za kuokoa mpira.
Laiti mabeki wa KMC wangekuwa makini kuokoa hatari ya Mapigano aliyoizuia ingekuwa ni bahati kwao kutofungwa na kwa upande wa Simba tatizo la uokoaji linaonekana kuwa kwenye mwendelezo kutokana na makosa kujirudia mara kwa mara.
Chuma cha tatu ni mali ya Inonga dakika ya 73 ni mara ya pili kufunga kwenye mechi mbili ndani ya ligi msimu wa 2022/23.
Bao lake la kwanza alifunga Uwanja wa Kaitaba wakati wakitoshana nguvu na Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1.