AZAM FC YATAJA SABABU YA KICHAPO

KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa walikwama kushinda mbele ya Yanga kutokana na kushindwa kuwa makini.

Azam FC jana Desemba 25 ilinyooshwa mbele ya Yanga kwenye mchezo wa ligi na kuyeyusha mazima pointi tatu.

aada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 2-3 Yanga ambapo bao la ushindi lilifungwa na Farid Mussa dakika ya 77 na kuipa ushindi timu yake ya Yanga ambao ni vinara wa ligi.

Ongala amesema:”Tulipoanza kuongoza ninadhani wachezaji walishindwa kuendelea kuongeza umakini na makosa ambayo tulifanya wapinzani wetu walifanikiwa kuyatumia.

“Makosa hayo tutafanyia kazi kwa ajili ya mechi zijazo kwa kuwa bado ligi inaendelea,”,