KUELEKEA kwenye uchaguzi mkuu wa Simba unaotarajiwa kufanyika Januari 29,2023 kamati ya uchaguzi jana Desemba 25,2022 imetoa orodha ya wagombea 14 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Boniface Lihamwike imebainisha kuwa majina ya waliopitishwa ni wale ambao wamekidhi vigezo huku idadi ya wanaowania nafasi ya mwenyekiti ikiwa na wagombea wawili, 12 kwa upande wa ujumbe na kukamilisha idadi ya majina 14 ya waliopitishwa.
Kwa upande wa wale wanaogombea nafasi ya mwenyekiti majina yao ni Adv.Moses Kaluwa na Murtanza Mangungu yamepenya.
Kwa majina ya wagombea nafasi ya Ujumbe Bodi ya Wakurugenzi ni Dkt Seif Ramadhani Muba, Seleman Said, Iddi Kitete, CPA(T)Issa Iddi, Abubakari Zebo, Abdallah Mgomba, Eng.Elisomy Mweladzi, Eng. Rashid Mashaka, Rodney Makamba, Aziz Mohamed, Asha Baraka na Pendo Aidan.
Ni nafasi moja ya mwenyekiti atachaguliwa huku kwa upande wa wajumbe ni wanne ambao watachaguliwa na wanachama pia kuna nafasi mbili za wajumbe ambao watateuliwa na mwenyekiti.