ZAWADI ya Chritmas imetolewa kwa mashabiki wa Yanga baada ya timu hiyo kutoka nyuma ilipoanza kufungwa na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mkapa na mwisho ukasoma Azam FC 2-3 Yanga.
Ni Abdul Seleman, ‘Sopu’ alianza kumtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra dakika ya 27 akitumia pasi ya Prince Dube pia alifunga bao la pili kipindi cha kwanza dakika ya 47.
Sopu mwenye rekodi ya kuwatungua Yanga hat trick kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho alipokuwa ndani ya Coastal Union alikwama kuyeyusha dakika 90 na nafasi yake ilichukuliwa na Ayoub Lyanga.
Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na kiungo Farid Mussa ambaye aliingia akitokea benchi dakika ya 73 alifunga bao hilo dakika ya 77 akitumia makosa ya Ahamada ambaye alikwama kuokoa faulo iliyopigwa na Aziz KI.
Ikumbukwe kwamba hata msimu wa 2021/22 bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa dakika 77 na Mayele mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni rekodi inajirudia kwa mara nyingine Uwanja wa Mkapa.
Mabao mengine ya Yanga yallifungwa na Fiston Mayele dakika ya 31 alipachika bao hilo akitumia pasi ya kiungo Bernard Morrison na kabla hawajapoa Azam FC walikutana na balaa lingine la Aziz KI.
Ki alipachika bao hilo dakika ya 32 kwa pasi ya Khalid Aucho akiachia shuti kali akiwa nje ya 18 likamshinda kipa namba moja wa Azam FC, Ali Ahamada mwenye umbo lililojaa kutokana na mazoezi.
Dakika 45 za mwanzo mwamuzi wa kati Joachim Akamba hakutoa onyo kwa kuwaonyesha kadi wachezaji wote licha ya matumizi ya nguvu kwenye mchezo huo lakini kipindi cha pili mwamuzi alionesha kadi za njano huku mchezaji wa kwanza akiwa ni Salum Aboubhakari, ‘Sure Boy’ dakika ya 53 na kwa Azam FC ni Sospete Bajana alikuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 76.