KAZI IPO KESHO UWANJA WA MKAPA

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa dabi ya Kariakoo upande wa Wanawake, Simba Queens v Yanga makocha wote wameweka wazi kwamba wapo tayari kwa mchezo huo.

Simba Queens ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Wanawake Tanzania watawakaribisha Yanga Princess Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Yanga Princess ambaye ameibuka hapo muda mfupi baada ya kuachana na mabosi zake wa zamani Simba Queens ameweka wazi kuwa hautakuwa mchezo rahisi:

Sebastian Nkoma amesema kuwa anatambua amepokea kikosi muda mfupi lakini haina maana kwamba atashindwa kusaka ushindi

“Hautakuwa mchezo rahisi kwa timu zote mbili, nilikuwa mwalimu wa Simba Queens na ninawafahamu wachezaji wao na wao wananifahamu, hivyo hautakuwa mchezo mwepesi.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwenye mchezo wetu ambapo timu bado haijawa kweye ubora wake kwa muda huu mfupi lakini tutafanya kazi kubwa kusaka ushindi,”.

Kwa upande wa Charles Lukula, Kocha Mkuu wa Simba Queens amesema kuwa wanatambua mchezo hautakuwa mwepesi wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.

“Moja ya mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa kwa mbinu tupo tayari na tutafanya kazi kubwa kutafuta matokeo,”.