KIUNGO wa zamani wa Yanga, Simba na Azam FC Ibrahim Ajibu anatajwa kumalizana na mabosi wa Singida Big Stars.
Nyota huyo uora wake aliokuwa nao Yanga alipomaliza kwa kutoa pasi 17 za mabao bado anautafuta kwa kuwa hajagotea namba hata 10 ya pasi za mwisho.
Kwa sasa mzee wa makorokocho anatajwa kutua ndani ya Singida Big Stars kwa dili la miaka miwili.
Ndani ya Azam FC msimu huu wa 2022/23 hajaonyesha makeke kutokana na kutopewa nafasi kikosi cha kwanza.
Mchezo pekee alioonekana ni ule dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu ubao uliposoma Mtibwa Sugar 3-4 Azam FC.
Mabosi wa Azam FC wamemuaga rasmi kwa kusema asante Ibrahim Ajibu kuwa kwenye familia yetu.