SIMBA KAMILI KUIVAA KAGERA SUGAR KAITABA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar maandalizi yake yapo sawa kinachosubiriwa ni dakika 90.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Inakutana na Kagera Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Kaitaba.

Mgunda amesema:”Maandalizi kuhusu mchezo wa Kagera tumefanyia kazi na ninajua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini tupo tayari kwa ushindani,”.