AZAM FC KUKIPIGA NA COASTAL, KIINGILIO JEZI

NOVEMBA 27,2022 Azam FC itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Katika mchezo huo kiingilio ni uzi wa Azam FC kwa yule ambaye hana jezi hiyo akifika uwanjani watafanya mazungumzo kujua shughuli inakwendaje.

Azam FC imekuwa kwenye mwendo mzuri msimu huu baada ya kutoka kuinyoosha bao 1-0 Namungo ikiwa ugenini.

Kali Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanaamini mchezo ujao utakuwa mgumu.

“Tutakuwa nyumbani lakini mechi zetu zote zina ushindani mkubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu,”.