GEITA GOLD YAIPIGIA HESABU IHEFU

BAADA ya kucheza mechi 13 Geita Gold yenye Said Ntibanzokiza ambaye ni kiungo mshambuliaji imekusanya pointi 18.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya tano na ni mechi nne imeshinda imeambulia kichapo kwenye mechi tatu na sare kibindoni ni sita.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Ihefu ambao unatarajiwa kuchezwa Novemba 25.

Geita Gold watakuwa nyumbani pale Uwanja wa Nyankumbu kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Watawakaribisha Ihefu chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye ameweka wazi kuwa kila mchezo kwao ni muhimu kupata pointi tatu.

Kwenye msimamo Ihefu ipo nafasi ya 16 baada ya kucheza mechi 12 imekusanya pointi 8.