KIUNGO wa Simba Peter Banda ataukosa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting kwa kuwa bado hajawa fiti.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wanatambua wanakwenda kukutana na timu ngumu.
“Kila kitu kuhusu mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting kimekamilika na tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu tupo tayari.
“Peter Banda bado hajawa fiti baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars pia hata Israel Mwenda na mwanangu Jimsone bado hawajawa fiti lakini ninamshukuru Mungu wanazidi kuimarika,”.
Simba imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu inakutana na Ruvu Shooting ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.