NOVEMBA 15,2022 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa wababe kuendelea kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90.
Ni KMC hawa watoza ushuru wao watamenyana na Dodoma Jiji utachezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.
KMC kibindoni wana pointi 14 wanakutana na Dodoma Jiji wenye pointi 6.
Azam fc V Ruvu Shooting hawa watamenyana Uwanja wa Azam Complex.
Ni pointi 23 wanazo Azam FC huku Ruvu Shooting wakikusanya pointi 11 kibindoni.